Wacheza shoo wa Mashujaa wakiwa kazini |
Add caption |
Charles Baba akiwa amepiga amechuchumaa wakati akimvika pete ya uchumba Rehema Sospeter |
BENDI ya Mashujaa jana usiku ilikata kiu ya mashabiki wa
muziki wa dansi baada ya kutoa burudani iliyo konga nyoyo za wadau kwenye
ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
Mashujaa walikuwa wanatambulisha albamu yao ya Risasi Kidole
kwa mashabiki wao walisindikizwa na FM Academia bendi chini ya rais wao Nyoshi
el Sadaat pia walitoa burudani nzuri.
Kwenye onyesho hilo FM Academia ndio walikuwa wa kwanza
kupanda jukwaani na kutoa burudani nzuri na wakafuatiwa na Mashujaa ambao nao
walitoa burudani ya nguvu bila kusimama.
Mashabiki walionekana kufurahia dansi kwani muda wote
walikuwa wamesimama wakicheza na kuwatunza wacheza shoo na waimbaji.
Mkurugenzi wa Mashujaa Bendi, Sakina Mohmed Mbange maarufu kama Mama Sakina hakuwa nyuma
kuonyesha furaha yake kwani alikuwa anacheza muda wote huku akifurahi hadi
kutokwa na machozi.
Rais wa bendi ya Mashujaa, Charles Baba alimtambulisha mpenzi
wake Rehema Sospeter kwa mashabiki na kumvisha pete ya uchumba na kusema ndie mke wake
mtarajiwa na sasa wapo kwenye maandalizi ya kufunga ndoa.
No comments:
Post a Comment