Pages

Sunday, May 12, 2013

AZAM YAKATA TIKETI YA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO MWAKANI BAADA YA KUIFUNGA MGAMBO 3-0



TIMU ya Azam  leo imeifunga Mgambo Shooting mabao 3-0 na kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani,  katika  mchezo  mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi  51, huku ikiikaribia Yanga yenye ponti 55, ambapo kila timu imebakisha mchezo mmoja.
Azam FC walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa  bao 1-0, lililofungwa na John Bocco dakika ya 23 baada ya kupokea pasi kwa  Humphrey  Mieno.

Kipindi cha pili, Azam walirudi na kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 65 lililofungwa na Kipre Tchetche baada ya kuwapiga chenga wapinzani na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Mgambo Shooring FC.
Bao la tatu lilifungwa na Joackins Atudo baada ya kuunganisha kwa kichwa kona ya Erasto Edward Nyoni dakika ya 80 na mpira ukatinga nyavuni.

Azam watacheza tena michuano ya Shirikisho mwakani, baada ya mwaka huu kutolewa Raundi ya Tatu na AS FAR Rabat ya Morocco wakishiriki kwa mara ya kwanza.
Kikosi cha Azam: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk85, Kipre Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Abdi Kassim dk83 na Brian Umony/Seif Abdallah dk63.

JKT Mgambo; Tony Kavishe, Salum Mlima, Ramadhani Malima, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Mussa Gunda, Juma Mwinyimvua/Peter Mwalyanzi dk 56, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.

No comments:

Post a Comment