TIMU ya Azam leo
imeifunga Mgambo Shooting mabao 3-0 na kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza
michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, katika mchezo mchezo
wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam.
Kwa matokeo hayo Azam imefikisha pointi 51, huku ikiikaribia Yanga yenye ponti 55,
ambapo kila timu imebakisha mchezo mmoja.
Azam FC walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0, lililofungwa na John Bocco dakika ya
23 baada ya kupokea pasi kwa Humphrey Mieno.
Kipindi cha pili, Azam walirudi na kasi na kufanikiwa kupata
bao la pili dakika ya 65 lililofungwa na Kipre Tchetche baada ya kuwapiga
chenga wapinzani na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango wa Mgambo Shooring
FC.
Bao la tatu lilifungwa na Joackins Atudo baada ya kuunganisha
kwa kichwa kona ya Erasto Edward Nyoni dakika ya 80 na mpira ukatinga nyavuni.
Azam watacheza tena michuano ya Shirikisho mwakani, baada ya
mwaka huu kutolewa Raundi ya Tatu na AS FAR Rabat ya Morocco wakishiriki kwa
mara ya kwanza.
Kikosi cha Azam: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum,
Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk85, Kipre
Tchetche, Salum Abubakar, John Bocco, Humprey Mieno/Abdi Kassim dk83 na Brian
Umony/Seif Abdallah dk63.
JKT Mgambo; Tony Kavishe, Salum Mlima, Ramadhani Malima,
Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Mussa Gunda, Juma
Mwinyimvua/Peter Mwalyanzi dk 56, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo.
No comments:
Post a Comment