Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 12, 2013

BREAKING NEWS!!!!!!! ROBERT MAANCINI ATIMULIWA MAN CITY, SASA NAFASI YAKE KUCHUKULIWA NA PELLEGRINI

Mancin
Pellegrini

BAADA ya jana Manchester City kupata kipigo  toka kwa Wigan kwenye mchezo wa kombe la FA Robert Mancini ametimuliwa kibarua chake

Mancini pamoja na kuwa alisaidia City kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Kombe la FA na kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu imevuliwa makombe yote msimu huu na uliopita.
Nafasi ya Mancini huenda ikachukuliwa na Pellegrin kwani uongozi wa City inasemekana ulikutana na wakala wake wiki mbili zilizopita na uongozi wa City haukuonyesha juhudi za kukanusha kwamba ulikutana na wakala wa Pellegrin na aliyefanya naye mazungumzo ni Txiki.

Taarifa za Txiki kukutana na wakala wa Pellegrini zilianza kuchukua nafasi tokea wiki iliyopita na uongozi wa City ulionekana kuwa kimya kabisa kuhusiana na suala hilo.
Bado haijajulikana rasmi ataondoka leo usiku, kesho au keshokutwa lakini inaonekana hakuna uhakika kama atakuwepo kwenye benchi kesho wakati City watakapokuwa wakiivaa Reading.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Man City zinaeleza, uamuzi wa kumtimua Mancini ulichukuliwa katika kikao cha pamoja kilichowajumuisha mabosi wawili Ferran Soriano, Txiki Begiristain na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak ikiwa ni siku moja tu baada ya City kuchapwa bao 1-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la FA.

The Sun la Uingereza lilifanya juhudi za kumnasa Mancini ili azungumzie suala hilo lakini haikuwezekana lakini kumekuwa na taarifa amebanwa kwa kuwa anashughulikia suala la malipo ya fedha zake baada ya mkataba wake kusitishwa.

Ingawa yeye alisema jana amebakiza miaka minne na City, lakini taarifa zinaeleza ana miaka mitatu iliyosalia na alisaini baada ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England.

No comments:

Post a Comment