Pages

Sunday, May 19, 2013

ATLETICO YAINYUKA MADRID NA KUTWAA KOMBE LA MFALME

MADRID, Hispania
ATLETICO Madrid imetwaa taji lake la 10 la Copa del Rey, baada ya mabao mawili kutoka kwa Diego Costa na Miranda kuwasaidia kuwafunga mahasimu wao Real Madrid 2-1, katika muda wa nyongeza, fainali ambayo iliwashuhudia Jose Mourinho na Cristiano Ronaldo wakionyeshwa kadi nyekundu.

Real Madrid ilikuwa haijafungwa kwa mechi 25 dhidi ya mahasimu wao hao na kikosi hicho cha Mourinho kilianza vyema kwa bao la Cristiano Ronaldo, aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Luka Modric.

Lakini, Diego Costa alisawazishia Atletico dakika 10 kabla ya mapumziko na Los Rojiblancos kisha wakanusurika hatari kadha baada ya mashuti ya Mesut Ozil, Karim Benzema na Ronaldo kugongesha mwamba.

Mourinho alitolewa kwa kadi nyekundu dakika 77, kutokana na kuonekana kugomea maamuzi na baadaye Miranda kufunga kwa kichwa kuifanya Atletico kufunga bao la pili dakika nane baada ya muda wa nyongeza.

Kasheshe zaidi ilikuja baadaye, baada ya Ronaldo naye kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Gabi, zikiwa zimesalia dakika sita tu kabla ya filimbi ya mwisho.
"Tulipata nafasi mbili za wazi za kufunga, tuligongesha mwamba mara tatu, hii ndiyo maana nasema haipo sawa," alisema Mourinho.

No comments:

Post a Comment