Pages

Wednesday, April 17, 2013

YANGA YANUSURIKA KUFUNGWA NA MGAMBO JKT MKWAKWANI, MSUVA AIKOA DAKIKA ZA LALA SALAMA




TIMU ya Mgambo JKT leo imetoshana nguvu na Yanga baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Yanga ambayo ilifanya kazi ya kusawazisha kupitia kwa Simon Msuva dakika ya 86 ilianza kufungwa na Mgambo JKT walijipatia bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Issa Kanduru baada ya kupokea pasi toka kwa Salum mlima
Kwa matokeo hayo Yanga SCimefikisha pointi 53 ikiwa bado kileleni ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 47.
Kikosi cha Mgambo JKT:  Godson Mmasi, Salum Mlima, Juma Roisana/Yassin Awadh, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja/Omar Matwiko, Mussa Mgunda, Issa Kanduru, Fulla Maganga na Nassor Gumbo.

Yanga SC; Ally Mustafa, Mbuyu Twite, Oscar Joshua/Haruna Niyonzima, Nadir Haroub, Kevin Yondan, Athumani Iddi, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi, Nizar Khalfan na David Luhende.


No comments:

Post a Comment