Pages

Sunday, April 21, 2013

BONDIA HAMIS AJALI APIGWA KWA KO NA DJAMEL DAHOU WA ALGERIA

Bondia Djamel Dahou akipambana na Hamis Ajali kwenye pambano Ubingwa wa Afrika UBO uzito wa Light Welter Weight lililofanyika ukumbi wa DDC Keko jijini Dar es Salaam jana


Hapa wanaonyeshana uwezo wa kurushia makonde

Wamesimama kuimba Wimbo wa taifa la Algeria

Wimbo wa taifa la Tanzania unaimbwa

Bondia Djamel Dahou akisujudi baada ya kushinda kwa KO

Mwamuzi anamtangaza rasmi kuwa bingwa wa UBO Afrika  uzito wa Light Welter Weight


Balozi wa Algeria hapa nchini Djelloul Tabet (aliyevaa miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja baada ya pambano kumalizika.

BONDIA Hamisi Ajali jana alipigwa kwa technical knockout (KO) na bondia Djamel Dahou wa Algeria kwenye pambano la Ubingwa wa Afrika Light Welter Weight la raundi 10, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Keko, jijini Dar es Salaam.

Ajali alikumbana na kadhia hiyo kwenye raundi ya pili baada ya kupigwa konde lililompeleka chini na kushindwa kusisima ndipo Djamel Dahou alipojichukulia mkanda wa UBO ndani ya dakika nne tu.

Kitendo cha bondia Ajali kupigwa kwa KO kwenye hatua za awali kilionyesha kuwakasirisha mashabiki wa mchezo huo waliokuwa wamefurika kushuhudia

Alisikika shabiki mmoja akisema kuwa Ajali kuwa amewatia aibu kupigwa mapema na sasa hawajui waende wapi ili kuupoza machungu kwani ni mapema, ilikuwa saa tatu .

Awali akizungumza kabla ya pambano hilo kuanza mgeni rasmi ambaye alikuwa balozi wa Algeria hapa nchini Djelloul Tabet aliwaasa mabondia kucheza kwa kufuata kanuni za mchezo huo pia aliwakumbusha kuwa michezo hujenga urafiki.

“Michezo hujenga urafiki hivyo mfuate kanuni mnapokuwa ulingoni kwani Tanzania na Algeria ni marafiki hivyo na nyie ipo siku mtakwenda Algeria kucheza”, alisema Tabet.

Kabla ya pambano hilo kuanza yalichezwa mapambano sita ya utangulizi ambapo Kassim Gamboo alimpiga Shabani Mkala kwa pointi tatu kwa bila pambano la raundi nne uzito wa Bantaweight na Joseph Mpilimi alimpiga Kaisi Rashid kwa pointi mbili kwa moja kwenye uzito wa Lightweight.

Naye Haji Juma wa Tanga alimpiga kwa KO raundi ya tano Mohamed Mzungu kwenye uzito wa Bantamweight la raundi sita na Ibrahim Tamba alipewa ushindi kwa mpizani wake Doto Kipacha hakutokea ulingoni.

Amos Mwamakula alimpiga Jumanne Mohamed kwa KO raundi ya pili kwenye pambano la sita uzito wa Light welter na Juma Fundi alimpiga Abuu Mtambwe kwa pointi tatu kwa sifuri kwenye pambano la raundi nne uzito wa Bantamweight.

No comments:

Post a Comment