Pages

Sunday, April 21, 2013

WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA SERENGETI BOYS SASA KUWA WACHEZAJI WA TIMU YA U-20










TIMU ya Taifa ya Vijana walio chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti boys imepandishwa na kuwa kuwa timu ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 20.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO, Kocha wa timu hiyo Jacob Michelsen alisema kuwa wachezaji hao wamepandishwa kuwa timu ya Taifa ya vijana ya miaka 20 baada ya kuonekana umri wao unakaribia kufikia kikomo hivyo kutokana na uwezo wao kuwa mzuri ndio maana wamepandishwa ili waendelee kulitumika taifa.

“Ili kuwa mchezaji wa timu ya Serengeti boys unatakiwa umri usiwe umefik miaka 17 hivyo wengi wanafikisha miaka 17 mwaka huu ndio maana tumeamua kuwapeleka timu ya taifa U20”, alisema Jacob.

Pia kikosi cha wachezaji wa timu iliyokuwa ya U-20 wapendishwa kwenye kikosi cha U-23 ambayo itakuwa inatumika kama timu ya taifa Taifa stars B

Miongoni mwa wachezaji hao ni Miraji Seleman ambaye alikuwa nahodha, Seleman Bofu, Ismail Gambo, Husein Twaha, James Mganda, Miza Abdallah, Mudathiri Yahya,Farid Mussa na Mohamed Haroub.
Wengine ni Abdallah Bakari, Abdallah Salum, Mgaya Abdul, Mohamed Musa, Pascal Matagi, Mzamiru Said na Dickson Ambunda

Wachezaji walioko kambini ni 27 kwa ajili ya mazoezi ya program ya wiki moja na kambi itafungwa jumapili baada ya kucheza mchezo wa kirafiki wao kwa wao.

No comments:

Post a Comment