Pages

Sunday, April 21, 2013

ALEX FERGUSON ATUPILIA MBALI TAARIFA ZA ROONEY KUELEKEA PSG.


Wayne Rooney of Manchester United looks dejected after coming on as a second half substitute
Add caption

Ule uvumi kuwa Wayne Rooney yupo njiani kuhamia PSG uliopata kasi kubwa baada ya Juzi mmoja wa Washauri wa zamani wa Klabu hiyo, Michel Moulin, kudai Dili imeshakamilika, leo umetupiwa mbali na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson.

Michel Moulin, ambae sasa anamiliki Chombo cha Habari huko Ufaransa Le Sport 10, alitamka kwenye TV: “Natangaza kwenu kutoka vyanzo vya kuaminika Rooney kwenda PSG ishafanyika. Atakuwepo PSG Msimu ujao!”

Lakini leo, Sir Alex Ferguson, akihojiwa na Wanahabari alijibu: “Sidhani kama kuna lolote humo!”
Madai hayo ya kuhama Rooney yamekuwa yakipamba moto hasa baada ya Juzi Rooney kutolewa nje kwenye Mechi na West Ham na kubadilishwa katika Kipindi cha Pili lakini Sir Alex Ferguson amezungumza hilo kwa kusema: “Kuhusu kumbadili Kipindi cha Pili na West Ham ni rahisi kuelezea! Hakuwa anacheza vizuri kama Shinji Kagawa. Katika Mechi nyingi Rooney anacheza vizuri mno kupita Wachezaji wengi lakini Siku ile Kagawa alicheza vizuri zaidi.”

Man United v Aston Villa 
Akielezea hali ya Kikosi chake ambacho Juzi kilitoka sare ya Bao 2-2 na West Ham huko Upton Park, Sir Alex Ferguson alisema: “Tulitoka Uwanja wa Vita kama unavyotegemea toka kwa Timu za Big Sam [Sam Allardyce] lakini hatuna majeruhi licha ya michubuko kidogo na uvimbe hasa kwa Vidic.”

Pia Ferguson alithibitisha kuwa Kikosi kilekile kilichoikabili West Ham ndio atateua Wachezaji wake kuunda Timu ya kuivaa Aston Villa Jumatatu Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi muhimu ya BPL, Barclays Premier League, ambayo huenda ikawapa Ubingwa ikiwa Jumapili Man City watafungwa na Tottenham huko White Hart Lane na wao kuichapa Villa.

No comments:

Post a Comment