Pages

Thursday, April 25, 2013

RED COAST YAZIDI KUSHIKILIA USUKANI WA LIGI DAR ES SALAAM

Mshambuliaji wa Boom Fc Janker Ally akipiga shuti kwenye mchezo wa  ligi daraja la pili uliochezwa uwanjaw a Makurumla Kinondoni huku 

Beki Rashid Juma wa Red Coast (njano) akiwania mpira na Barnabas Kanji (red) kwenye mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa uwanja wa Makurumla jana.


TIMU ya Abajalo jana iliifunga Friends Rangers bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam hatua ya sita bora kwenye uwanja wa Kinesi.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kutokana na timu zote kucheza soka la uhakika lakini mabeki wa Friends Rangers waliruhusu bao la mapema lililofungwa na Waziri Omary katika dakika ya 35, bao ambalo lilidumu hadi mchezo kumalizika.

Kwenye Uwanja wa Makurumla, Boom FC ilitoka sare ya bao 1-1 na Read Coast mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia kutokna na timu zote kucheza soka la kushambuliana kwa zamu dakika zote.

Red Coast ndio walioanza kufunga bao kupitia kwa Idrisa Pandu dakika ya 28 na Boom FC wakasawazisha kupitia kwa Janker Ally katika dakika ya 41.

Uwanja wa Airwing, Sharif Stars iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Day Break, bao hilo lilifungwa na Dovan Kanyinda katika dakika ya 89.

Red Coast inaongoza ligi ikiwa na pointi 8 ikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 7 na Sharif Stars ina pointi 6  ambapo kila timu imecheza michezo minne na ligi hiyo itafikia tamati Aprili 27.

No comments:

Post a Comment