Pages

Thursday, April 25, 2013

GABADINHO AZIDI KUNG'ARA MALAWI



LILONGWE, Malawi
MCHEZAJI bora wa mwaka wa Malawi, Gabadinho Mhango, amethibitisha ubora wake baada ya kuingia akitokea benchi na kuiwezesha timu yake ya Big Bullets kutwaa ngao ya hisani kwa kuilaza Silver Strikers 3-1 mjini Lilongwe.

Gabadinho, aliyekuwa chachu ya mafanikio kwa timu yake msimu uliopita, alifunga bao katika mechi hiyo iliyokuwa ya pili kwa miamba ya soka nchini Malawi kukutana ambapo katika mechi ya kwanza ya kombe la Serikali wiki iliyopita alifunga bao pekee kwa Bullets.

Chipukizi huyo katika mchezo wa juzi aliingia kuchukua nafasi ya Diverson Mlozi katika dakika ya 78 na kufunga bao la tatu kwa timu yake na kuihakikishia ushindi Bullets na kuipa taji la pili ndani ya wiki mbili.

Katika mchezo huo Bullets, walicheza wakiwa pungufu baada ya beki wake, Sankhani Mkandawire kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 43, iliongoza kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 89 wakati Silver walipopata bao la kufutia machozi.

No comments:

Post a Comment