Pages

Sunday, April 28, 2013

RED COAST, ABAJALO NA FRIENDS RANGERS ZAFUZU KUCHEZA KANDA DAR ES SALAAM


Benjamini Mlowe wa Shafif Star (blue) akijaribu kumiliki mpira huku Khatibu Kuduku wa Friends Rangers akimzuia kwenye mchezo uliochezwa jana uwanja wa Makurumla Magomeni, Friends Rangers walishinda 2-0

Bakari Mlenge wa Friends Rangers akiwa na mpira

Halidi Badra akiwa na mpira wakati wa mchezo wa ligi daraja la pili uliochezwa uwanja wa Makurumla jana




TIMU za Red Coast, Abajalo na Friends Rangers zimefuzu kucheza hatua ya Kanda ya Dar es Salaam baada ya ligi daraja la pili kumalizika zikiwa zinaongoza kwenye nafasi tatu za mwanzo.

Ligi Daraja la Pili mkoa wa Dar es Salaam ambayo ilikuwa inachezwa kwenye ya hatua ya sita bora ilimazika juzi kwa mechi tatu kuchezwa kwenye viwanja vitatu.

Katika mechi iliyochezwa Makurumla, Friends Rangers iliifunga Sharif Stars mabao 2-0, mabao hayo yalifungwa na Khatib Kuduku katika dakika ya 12 na Mwenda Athuman katika dakika ya 57.

Uwanja wa Kinesi Red Coast waliibuka na  ushindi wa bao 1-0, lililofungwa dakika ya 32 na Rafael Mapunda.
Abajalo nao imefuzu baada ya kuichapa Boom FC mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Airwing lakini hata hivyo mechi hiyo ilivunjika kutokana na wachezaji watatu wa Boom FC kutolewa kwa kadi nyekundu na wengine kuumia na kushindwa kukidhi sheria 17 za soka.

 Red Coast imefuzu kwa kujikusanyia pointi 11 wakiwa vinara wa ligiikifuatiwa na Abajalo yenye pointi 10 na Rangers ikihitimisha baada ya kujikusanyia pointi 8.

No comments:

Post a Comment