Pages

Sunday, April 7, 2013

RAIS KIKWETE KUTUNUKIWA TUZO YA HESHIMA YA KANUMBA LEO


IMG-20130406-WA002Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ataongoza kundi la watu na taasisi kadhaa katika kupokea tuzo maalum za kumbukumbu ya msanii nguli nchini marehemu Steven Kanumba

Hafla ya utoaji tuzo hizi za shukrani, itakuwa ndio hitimisho la shughuli kadhaa zilizokuwa zimeandaliwa na familia ya marehemu Kanumba kwa kushirikiana na wadau wengine kadhaa katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja toka kufariki kwa msanii huyo.

Marehemu Kanumba, alifariki dunia tarehe kama ya leo mwaka jana akiwa nyumbani kwake kufuatia kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi baina yake na aliyekuwa mpenzi wake, Elizabeth Michael “Lulu”, ambaye pia aliungana na familia ya marehemu katika kumbukumbu hii iliyohusisha kuweka mashada ya maua kwenye kaburi la marehemu.

Wazo la tuzo hizo liliasisiwa na familia ya marehemu kwa lengo la kuwashukuru wale wote waliotoa mchango mkubwa katika kufanikisha mazishi ya marehemu pamoja na kuenzi mchango wa watunukiwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini.

Mpejiwa ambaye ndiye aliyeandaa tuzo zenyewe chini ya kampuni yao ya Point Inc. amesema kuwa mbali ya Rais Kikwete, wengine watakaokabidhiwa tuzo zao uziku huu ni kampuni za IPP Media, Clouds Media, Global Publishers, TAFF,Bongo Movie Club, Masoud Wanani, Millard Ayo, Game Fisrt Quality na Steps Entertainment.

Mwakilishi wetu huyo ameongeza kuwa, ingawa bado haijathibitishwa, zimekuwepo taarifa za kwamba tuzo hizo huenda zikawa zinatolewa kila mwaka kulingana na familia ya marehemu itavyoona inastahili na mawazo ya wadau wengine muhimu wa tasnia ya filamu nchini.

Picha chini, ni maandalizi ya shughuli yenyewe sehemu ya tukio

VN:F [1.9.22_1171]

No comments:

Post a Comment