Pages

Wednesday, April 3, 2013

PSG NA BARCELONA 2-2 NA BAYERN MUNICH NA JUVENTUS 2-0 :UEFA CHAMPIONS LEAGUE


PENATI YA BARCA YA UTATA YAWA MZIGO KWAO HUKU PSG WAKIWATUNISHIA KIFUA!!


ROBO FAINALI za UEFA CHAMPIONS LIGI, zimeanza kutimua vumbi jana usiku, Aprili 2, kwa Mechi mbili ambazo Barcelona walisafiri kwenda kucheza Uwanjani Parc des Princes na Paris Saint-Germain na Juventus kwenda huko Allianz Arena, Jijini Munich kucheza na Bayern Munich.Historia....Bao la mapema hivi...
Dream start: Bayern Munich's David Alaba (right) scored after 23 seconds against Juventus
Mchezaji wa Bayern Munich David Alaba (kulia) akifurahia baada ya kufunga bao la mapeema dakika ya kwanza (sekunde 23) kupita.

Lionel Messi akiifungia bao la kufungua kwa timu yake dhidi ya PSG

Lionel Messi akishangilia baada ya kupata bao dakika ya 38 kipindi cha kwanza.

Staa Beckham akiongeza nguvu ili waishinde Barcelona kushoto ni Dani Alves na David Villa (kulia)

Alaba akiwafungia bao la mapema Bayern Munich dakika ya kwaza na kipindi cha kwanza kuisha 1-0 dhidi ya Juventus huku Robben akikosa kufunga bao la wazi dakika ya 36 baada ya kuachia mkwaju mkali na kuokolewa na kipa. Kipindi cha pili dakika ya 63 mchezaji Mullerakawaandikia bao la pili Bayern na kufanya mpira umalizike 2-0 dhidi ya timu pinzani Juventus.
Doubling up: Thomas Muller taps Bayern Munich into a 2-0 lead
Thomas Muller akiwafungia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Juventus leo hii usiku
Doubling up: Thomas Muller taps Bayern Munich into a 2-0 lead
Wachezaji wa Bayern wakipongezana baada ya Thomas Muller kuwapatia bao la 2.
Wao Barcelona wamepata penati ya utata dakika ya 88 baada ya Alexis kujigusisha kwa kipa wa PSG Sirigu na mwamuzi kudai ni penati na mkwaju huo kupigwa na mchezaji Xavi na hatimaye kumuuza kipa na mpira kutokomea nyavuni upande wa pili na kufanya 1-2 dhidi ya PSG.

Paris Saint Germain nao hawakukata tamaa wakacheza na muda wa nyongeza kwa haraka na kwa makini. Dakika ya 90+4 Matuidi akatupiwa mpira na Ibra na hatimaye kutofanya makosa akaelekeza shuti kali golini mwa Barca na hatimaye kumkuta kipa wao akiwa ameanguka na kwa kujikuja miguu kwa ndani na mpira kumzidi nguvu kipa huyo Valdes.


RATIBA/MATOKEO - ROBO FAINALI
(Saa 3 Dak 45 Usiku)

Leo Jumanne Aprili 2
Paris Saint Germain 2 v Barcelona 2
Bayern Munich 2 v Juventus
0

Kesho Jumatano Aprili 3
Malaga v Borussia Dortmund
Real Madrid v Galatasaray

MARUDIANO
Jumanne Aprili 9
Galatasaray v Real Madrid
Borussia Dortmund v Malaga

Jumatano Aprili 10
Barcelona v Paris Saint Germain
Juventus v Bayern Munich

NUSU FAINALI
Mechi ya 1: Tarehe 23 na 24 Aprili 2013
Mechi ya 2: Tarehe 30 Aprili na 1 Mei 2013
FAINALI
25 Mei 2013
UWANJA WA WEMBLEY, LONDON

No comments:

Post a Comment