Pages

Wednesday, April 24, 2013

MBIO ZA KUMSAKA MRITHI WA REDS MISS TANZANIA, INDIAN OCEANS KAZI PEVU

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga akizungumza na warembo wanaoshiriki shindano la kumtafuta mshindi wa Redd's Miss Dar Indian Ocean wakati wa mazoezi yao kwenye ukumbi wa Bilicanas jijini Dar es Salaam.



HATUA za awali za kumsaka Redd’s Miss Tanzania sasa zinaanza kushika kasi, wakati wiki hii kutakapokuwa na kinyang’anyiro katika vitongoji kadhaa vya kusaka warembo wao.
 
Kazi kubwa itaanza Morogoro, wakati atakaposakwa Redd’s Miss High Learning atakayeuwakilisha mkoa huo katika kumpata mrembo kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu, shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sirvoy.
 
Wakati Morogoro Miss High Learning akipatikana kesho, shughuli pevu ipo keshokutwa (Jumamosi) pale kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s Miss UDOM, litakalofanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.
 
Siku hiyo pia atapatikana mwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Kagera na Mwanza, shindano ambalo litafanyika Yacht Club, Mwanza.
 
Akizungumzia kuhusu Redd’s Miss Morogoro High Learning, mratibu wa shindano hilo, Verdian Kamugisha alisema kila kitu kimekamilika na kutakuwa na burudani za kufa mtu.
 
“Tumekamilisha kila kitu na warembo wote wako katika hali nzuri na kutakuwa na burudani za kumwaga, wakazi wa Morogo wanatakiwa kuja kwa wingi kushuhudia kile kitakachotukia,” alisema.
 
Mratibu wa Shindano la Redd’s Miss UDOM, Rachel Matina naye alisema kila kitu kwao kipo tayari na watu wanatakiwa kufika kwa wingi kushuhudia jinsi warembo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, walivyopania kulitwaa taji la Redd’s Miss Tanzania mwaka huu.
 
Joseph Rwebangira wa anayeratibu shindano la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mikoa ya Kagera na Mwanza naye alikiri kukamilika kwa maandalizi yote na kutakuwa na burudani za kila aina siku ya onyesho.
Upande wa kanda ya kaskazini mwa nchi kutakuwa na shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Hai ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyikia katika ukumbi wa Hotel ya Snow View na mkoani Mara katika kitongoji cha Tarime shindano litakuwa katika ukumbi wa JJ Club na maandalizi kwa sehemu zote husika yameshakamilika kwa kiwango kikubwa.
 
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

No comments:

Post a Comment