Pages

Sunday, April 28, 2013

MANCHESTER UNITED YATOKA SARE NA ARSENAL KWA KUCHOMOA KUPITIA KWA ROBIN VAN PERSIE


MABINGWA Manchester United leo walitua Emirates kuchezea Mechi yao ya kwanza tangu wanyakue Ubingwa wa BPL, Barclays Premier League, na walipokelewa na Wachezaji wa Arsenal kwa Gwaride la Heshima kabla Mechi kuanza ikiwa pia ni Mechi ya kwanza kwa Nahodha wao zamani, Robin van Persie, kurudi Uwanjani hapo tangu awahame, Mechi ambayo ilimalizika kwa Bao 1-1 huku Van Persie akiifungia Man United bila kushangilia Bao lake. 

Wachezaji na mabingwa wa Ligi kuu England Manchester United wakiingia kwenye uwanja wa Arsenal leo hii jioni
Katika Mechi nyingine za awali hii leo, Chelsea iliichapa Swansea City Bao 2-0 na kukamata nafasi ya 3 na Reading na QPR kutoka sare ya 0-0 iliyoziteremsha Timu zote mbili Daraja.

Robin van Persie alifunga kwa Penati katika Mechi yake ya kwanza kucheza Uwanja wa Emirates tangu ahamie Man United kutoka Arsenal mwanzoni mwa Msimu huu katika Mechi ambayo ilimalizika sare ya Bao 1-1 matokeo ambayo si mazuri kwa Arsenal katika mapigano yao kufuzu katika 4 Bora kwani mapema Chelsea waliifunga Swansea na kuwapiku nafasi ya 3.
Pia Tottenham wako nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal lakini wana Mechi mkononi.
Arsenal ndio walitangulia kufunga katika Mechi hii katika Dakika ya pili baada ya pasi ya kutanguliziwa kumkuta Theo Walcott akiwa Ofsaidi ya wazi na kufunga Bao ambalo lilisimama kama lilivyo.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 44 kwa Penati iliyolewa na Refa Phil Dowd baada ya Bacary Sagna kumchezea Rafu Robin van Persie ambae yeye mwenyewe alifunga Penati hiyo bila kushangilia ikiwa ni heshima kwa Klabu yake ya zamani.
Hilo ni Bao la 25 kwa Van Persie katika BPL likimfanya aongoze kuwa Mfungaji Bora akifuatiwa na Luis Suarez mwenye Bao 23.
Theo Walcot akishangilia baada ya kuifungia bao timu yake ya Gunners ndani ya dakika mbili tu baada ya mchezo kuanza.What a start: Walcott soaks up the atmosphere after his clinical finish in the opening stages Walcott akishangilia bao lake la kwanza.Naye kipa wao Sczcesny aliitikia kwa furaha baada ya bao hiloVan Persie akifanya manjonjo yake leo hii wakati Man United wakiminyana na GunnersGooners: Jay-Z (left) and Chris Martin watch Arsenal's draw with Manchester UnitedMwana Muziki Jay Z na Chris Martin wakicheki mtanange wa Arsenal na Man UnitedSagna akifanya kitendo ambacho kimemwangusha RVP chini na Refa Phil Dowd kuamlisha upigwe na hatimaye Van Persie kupata bao la 25.RVP akipiga mkwaju wa penati.Kipa wa Arsenal Sczcesny hakuona ndani mkwaju huo maana RVP kaachia vya kutosha kukwepa kuumbuka.Mhhh....Kijana wetu katufunga..Wanajuana hawa Rooney na RVP wakipongezanaSczcesny amepata shida sana leo maana Van Persie alikuwa hatari sana leoWalcott na Evanc kidogo wakwaruzane hapa..VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Rosicky (Wilshere 62), Arteta, Walcott, Ramsey (Oxlade-Chamberlain 78), Cazorla, Podolski (Gervinho 71)
Subs not used: Mannone, Vermaelen, Monreal, Jenkinson
Booked: Sagna, Walcott, Oxlade-Chamberlain
Goal: Walcott 2
Manchester United: De Gea, Rafael (Anderson 73), Evra, Jones, Ferdinand, Evans, Valencia, Carrick, Nani (Giggs 83), Rooney (Hernandez 87), Van Persie
Subs not used: Lindegaard, Buttner, Cleverley, Kagawa
Booked: Rafael, Jones, Van Persie, Evans, Valencia
Goal: Van Persie 44 pen
Referee: Phil Dowd
Attendance: 60,112

No comments:

Post a Comment