Pages

Sunday, April 28, 2013

LIVERPOOL YATOA KIPIGO CHA PAKA MWIZI KWA NEWCASTLE KWA KUIFUNGA 6-0 BILA LUIZ SUAREZ


On the way: Daniel Agger (centre) scored early to put Liverpool on the way to a comfortable victoryWAKICHEZA Mechi yao ya kwanza bila Straika wao mkubwa, Luis Suarez, ambaye leo ameanza kutumikia Kifungo cha Mechi 10 kwa kumuuma meno Branislav Ivanovic wa Chelsea, Liverpool wakiwa ugenini Uwanjani St James Park, waliinyuka Newcastle Bao 6-0 katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League.


Mbali ya kipigo hiki kikubwa, Newcastle walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Mathiew Debuchy kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kumchezea Rafu Mbrazil Coutinho.
Matokeo haya yamewaacha Newcastle wakiwa nafasi ya 16 wakiwa Pointi 5 juu ya Wigan walio nafasi ya 18 ambao ni moja ya zile Timu za mwisho kwenye Msimamo wa Ligi na ambazo hushushwa Daraja mwishoni mwa Msimu.
Licha ya ushindi huu mnono, Liverpool imebaki nafasi yao ile ile ya 7 wakiwa Pointi 5 nyuma ya Mahasimu wao wakubwa Everton huku wote wakiwa wamebakisha Mechi 3.
Jose Enrique akichuana na Moussa Sissoko Sturridge akionekana kufurahi baada ya bao
Massadio Haidara akizuia mpira
VIKOSI:
Newcastle: Elliot, Debuchy, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Haidara, Sissoko, Tiote (Anita 65), Cabaye, Perch (Ben Arfa 46), Gutierrez (Gouffran 46), Cisse.
Subs Not Used: Harper, Williamson, Gosling, Ameobi.
Sent Off: Debuchy (75).
Booked: Debuchy, Gutierrez, Steven Taylor.
Liverpool: Reina, Johnson, Carragher, Agger, Jose Enrique, Henderson, Gerrard (Borini 72), Lucas, Coutinho (Suso 84), Sturridge (Shelvey 84), Downing.
Subs Not Used: Jones, Coates, Skrtel, Wisdom.
Booked: Sturridge, Johnson.
Goals: Agger 3, Henderson 17, Sturridge 54, 60, Borini 74, Henderson 76.
Att: 52,351
Ref: Andre Marriner  

No comments:

Post a Comment