Pages

Monday, April 29, 2013

LEWANDOWSKI AIPANDISHA PRESHA MNA UTD NA HABARI NYINGINE ZA KIMATAIFA

ROBERT LEWANDOWSKI amezidi kumpandisha presha Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson baada ya kukiri kwamba ana nafasi ya kumnasa baada ya Mario Goetze kutua Bayern Munich.

Kocha huyo wa Manchester United, wiki iliyopita aliweka wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Klabu yake kukataa kumuuza Mpoland huyo, hasa kutokana na Goetze kuwa tayari kutua Bayern Munich kwa pauni milioni 32.

Fergie alisema: “Mashabiki wa Dortmund hawatakuwa na furaha kuhusu Goetze na sidhani kama watamuuza Lewandowski kwa Bayern Munich kwa sasa. Nina nafasi yake? Ninaweza kutafuta nafasi kwa yeyote yule.”
@@@@@@@


Ferguson: Scholes anaweza kustaafu
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa Paul Scholes akatundika daluga mwishoni mwa msimu. Scholes, 38, amekuwa akikabiliwa na majeraha mara kwa mara msimu huu.
“Tutaona itakavyokuwa. Amekumbwa na majeraha na yamekuwa yakimkera sana," alisema Ferguson. “Atakuwa hapa mwaka ujao haijalishi ni mchezaji ama kocha.
“Utafika wakati ambao ni lazima aachie ngazi, lakini bado anayo mengi yakutupa.”
 @@@@@@@@

Di Canio amtaka Suarez asiondoke Liverpool
KOCHA wa Sunderland, Paolo di Canio amemtaka Luis Suarez kuendelea kuitumikia Liverpool na kudhihirisha tabia yake kwa wanaomkosoa.
Di Canio alisema: "Hawezi kunipiku mimi, kwani nilikuwa na mechi 11 ambazo nilipata wakati mgumu kwa kutaniwa!
"Ninatumai ataendelea kubaki England na kujaribu kuelewa kwamba huwezi kung'ata mkono wa mtu."
@@@@@@@@

Loic Remy kumrithi Suarez Liver
LIVERPOOL ipo tayari kutoa ofa ya pauni milioni 8 kwa Mshambuliaji wa QPR, Loic Remy wakati huu ambao inajiandaa kuingia msimu mpya bila Luis Suarez.
Liverpool bado inaamini kuwa haitaweza kumzuia raia huyo wa Uruguay kutimka nje ya England katika usajili wa majira ya joto.
Suarez, ambaye amefungiwa mechi 10 na hivyo sasa kulazimika kukosa michezo yote iliyobaki msimu huu baada ya kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic, pia atakosa mechi sita za mwanzo za msimu ujao.

@@@@@@@@
Spurs yamtaka Soldado wa Valencia
Tottenham imepiga hatua katika mpango wao wa kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Kihispania, Roberto Soldado wakati huu ambao Mwenyekiti wao, Daniel Levy akitaka kumtafutia wasaidizi Gareth Bale ili kuweza kutoa upinzani wakutosha msimu ujao.
Spurs ilitarajiwa kuwa kati ya watazamaji ambao wangehudhuria mechi kati ya Valencia na Real Sociedad, lakini lengo lao likiwa ni kumtazama Soldado, 27 wa Valencia.
@@@@@@@@

 Wenger amtaka Iker Casillas
Arsene Wenger  anamatumaini makubwa ya kuimiliki huduma ya Kipa namba moja wa Hispania, Iker Casillas na tayari amemweka kama chaguo lao namba moja kuelekea usajili wa majira ya joto, limeandika Gazeti la the Sunday People.
Kipa huyo wa Real Madrid hakubaliki na Kocha wa miamba hiyo ya Bernabeu, Jose Mourinho na kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dortmund wiki iliyopita ambayo alicheza na kuruhusu mabao manne, alikuwa hajachezeshwa tangu Januari.
Kocha wa 'Gunners', Wenger amejaribu kurusha ndowana kama anaweza kupata saini ya kipa huyo, 31, ambaye hajawahi kucheza klabu nyingine tangu aanzie soka lake Ashburton Grove.
@@@@@@@@@@@

Jovetic awekwa kiporo Fiorentina
RAIS wa Fiorentina, Mario Cognigni amekiri kwamba ofa nyingi zinatarajiwa kutua kwa mshambuliaji wao, Stevan Jovetic. Mshambuliaji huyo ni mmoja kati ya wachezaji wanaowindwa sana na Arsenal.
"Jovetic ni mwenye furaha hapa Florence,” Cognigni alisema. “Kama tulivyosema mwanzoni, tutakaa naye na kujadili mustakabali wake wa baadaye mwishoni mwa msimu.
“Lakini, hadi sasa, Jovetic ataendelea kufikiria kuhusu Fiorentina tu.”
 @@@@@@

Wiki muhimu kwa Kaizer Chiefs
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
KAIZER Chiefs jana ilianza wiki muhimu ambayo ndiyo itakuwa na mechi mbili zitakazotua mwanga kwa timu hiyo, kama itatwaa ubingwa wa soka nchini Afrika Kusini mapema au italazimika kusubiri hadi dakika za mwisho.
Chiefs jana ilikuwa kibaruani ikiwakaribisha moja ya wapinzani wao katika mbio za kuwania ubingwa huo, Platinum Stars katika mchezo ambao ni muhimu kwa timu zote hasa kwa kuwa Chiefs walihitaji ushindi ili kujiimarisha kileleni, lakini Platinum walihitaji ushindi ili kupunguza pointi.
Platinum wana pointi 49 katika nafasi ya pili huku Chiefs wakiwa kileleni kwa kuwa na pointi 55, hivyo pambano hilo lilikuwa na umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili kushinda kwa kila mmoja ingenufaika zaidi na ushindi katika mechi hiyo.
Mbali na mchezo huo, mechi  nyingine muhimu kwa Chiefs ni ile ya mahasimu wao wa jadi Orlando Pirates, ambayo itacheza na Chippa united hapo kesho, ambapo  endapo Pirates watapoteza au kutoka sare basi ni wazi kwamba, Chiefs watakuwa na nafasi kubwa ya kutawazwa mabingwa wapya wa soka nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment