Pages

Friday, April 26, 2013

ISHA MASHAUZI ADAIWA KUIBA 700,000 DUKANI KARIAKOO


MKURUGENZI wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani “Mashauzi” amelalamikia kitendo cha kudaiwa kuiba Laki 7 dukani kwa mtu anayejulikana kwa jina la Halima na kulazimika kusota rumande kwa madai kimepangwa ili kumdhalilisha kwenye fani yake ya uimbaji wa taarabu, huku akimiliki kundi la Mashauzi Classic.

Isha Mashauzi, mwimbaji wa taarabu na Mkurugenzi wa Mashauzi Classic

Isha alifikishwa kituo cha Msimbazi kwa kuhusishwa na upotevu wa shilingi laki saba uliotokea kwenye duka moja la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 
Mmiliki wa duka hilo la nywele, amemfikisha Isha na mwenzake aitwae Halima kituoni hapo akidai alipotelewa na kiasi hicho cha pesa huku msanii huyo akiwa ni wa mwisho kuingia dukani mwake.
 
Lenzi ya Michezo ilishuhudia pilika pilika za super star huyo kushikiliwa kwa muda saa 5 za usiku juzi huku mwimbaji huyo wa ‘Nani Kama Mama’ akisubiriwa na kamera za waandishi kwa nje.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Isha alisema alifika dukani kwa dada huyo Jumamosi iliyopita lakini baada ya kukosa alichokifuata aliingia duka lingine na kuliacha gari lake jirani na duka hilo lakini si kweli kama ameshiriki kwenye wizi huo.
 
Wakati anarudi kwenye gari lake, wafanyakazi wawili wa duka hilo wakamfuta na kumwambia kuna upotevu wa pesa umetokea.
Isha alisema baada ya mjadala wa muda mrefu akaawachia namba ya simu na kuwaambia iwapo bado watahitaji ufafanuzi zaidi wawasiliane.
 
“Kuanzia Jumatatu alianza kunipigia simu za vitisho na kuniambia atanikomesha na kunidhalilisha, hivyo nilipoona hali imezidi kuwa mbaya nikaenda kituo cha Msimbazi kuripoti juu ya vitisho vyake, ila cha ajabu kituoni nikanyimwa ushirikiano na kuamua kwenda Kinondoni ambapo ninaishi.
 
“Nikawaambia nimekuja Msimbazi kwa vile biashara ya mtu anayenipa vitisho hivyo ipo Kariakoo, lakini bado walikataa kunihudumia,” alisema Isha.
Kwa mujibu wa Isha, aliamua kujipanga aende kituo cha Oysterbay lakini leo (jana) nikapigiwa kutoka Msimbazi kuwa nifike kituoni hapo, ambapo nilipofika nikawekwa chini ya ulinzi kwa tuhuhuma za wizi wa shilingi laki 7.

Alisema baada ya kusota kwa masaa aliruhusiwa lakini akitakiwa kurudi tena kituoni hapo siku inayofuata, ambapo watu mbalimbali walijitokeza kumchukulia dhamana, akiwapo mtangazaji wa Times FM, Dida Shaibu.

No comments:

Post a Comment