Pages

Friday, April 26, 2013

CHELSEA YAIFUNGA FC BASEL 2-1 NA BENFICA NA FENERBAHCE ZATOKA SARE KWENYE MCHEZO WA EUROPA LEAGUE

YALE MASHINDANO YA NGAZI YA PILI KWA KLABU BARANI ULAYA, EUROPA LIGI, Usiku huu yameshuhudia Mechi zake za kwanza za Nusu Fainali kwa Chelsea kunyakua ushindi wa Bao 2-1 ugenini dhidi ya FC Basel ya Uswisi na Fenerbahce kupata ushindi wa Bao 1-0 Nyumbani walipoifunga Benfica ya Ureno.
Mechi za Marudiano ni Alhamisi ijayo.
EUROPA LIGI - NUSU FAINALI:
MATOKEO:
Alhamisi Aprili 25
 

FC Basel 1 Chelsea 2
Fenerbahce 1 Benfica 0


BASEL 1 CHELSEA 2
Uwanja: St-Jakob Park, Basel, Uswisi


David Luiz akiachia shuti kali na kuingia nyavuni usiku huu

Luiz akishangilia baada ya kufunga bao kwa frii kiki dakika ya lala salama dakika ya 90

Majanga: Luiz akimpelekea kiatu mguuni mchezaji wa Basel FC Philipp Degen

Fabian Schar akifunga penati dakika za mwishoni
Bao la Dakika ya 94 kwa frikiki ya David Luiz limewapa Chelsea ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya FC Basel ambao nao walisawazisha Bao Dakika ya 87 kwa Penati tata iliyopigwa na Fabian Schar kufuatia Fulbeki Cesar Azpilicueta kumkabili Valentin Stocker.
Chelsea walitangulia kufunga kwa Bao la Victor Moses katika Dakika ya 12 kufuatia Kona ya Frank Lampard kumparaza Branislav Ivanovic kichwani na, kibahati, kumgonga Moses kichwani na kutinga.Kocha wa muda wa Chelsea Rafa Benitez
VIKOSI:
Basle: Sommer, Philipp Degen, Schar, Dragovic, Park, Fabian Frei, Salah, El-Nenny, Die, Stocker, Streller.
Subs: Vailati, David Degen, Diaz, Cabral, Sauro, Steinhofer, Zoua.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Terry, Cole, Luiz, Hazard, Ramires, Lampard, Moses, Torres.
Subs: Turnbull, Mata, Oscar, Mikel, Cahill, Benayoun, Bertrand.
Ref: Pavel Kralovec (Czech Republic) 






FENERBAHCE v BENFICA
Uwanja: Sukru Saracoglu Stadium, Istanbul, Uturuki
Bao la Dakika ya 72 la Egemen Korkmaz limewapa Fenerbahce ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Benfica lakini, pengine, watajutia kukosa Penati iliyopigwa na Cristian na kugonga Posti ya chini na kutoka.


Kocha wa Benfica Jorge Jesus
Wamekutana hawa ndugu - Raul Meireles (left) and Dirk Kuyt (right) both played for Fenerbahce
Artur akiondoa mkwaju wa penati nje

Penati hiyo ilitolewa baada ya Gokhan Gonul kuangushwa na Ola John ndani ya Boksi.Mchezaji Korkmaz akiwakusanya wenzake kushangilia baada ya kufunga bao

VIKOSI:
Fenerbahce: Demirel, Gonul, Yobo, Korkmaz, Ziegler, Meireles (Ucan 64), Topal, Kuyt, Cristian (Sahin 86), Sow (Krasic 87), Webo.
Subs Not Used: Gunok, Irtegun, Senturk, Topuz.
Booked: Cristian, Topal, Webo.
Goals: Korkmaz 72.
Benfica: Artur Moraes, Maxi Pereira, Jardel, Garay, Melgarejo, Gomes (Carlos Martins 81), Aimar (Gaitan 46), Matic, John (Rodrigo 64), Cardozo, Salvio.
Subs Not Used: Paulo Lopes, Roderick Miranda, Lima, Urreta.
Booked: Gomes, Aimar, Maxi Pereira, John.
Attendance: 51,000
Referee: Milorad Mazic (Serbia).

No comments:

Post a Comment