Pages

Sunday, April 28, 2013

HARUNA NIYONZIMA: NIPENI DAU

Kama mabondia vile Niyonzina, Taita na Kiiza wakiwa wamevaa gloves boxers



Haaruna Niyonzima akifanya mazoezi gym jana

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema sasa anakaribisha mazungumzo ya mkataba mpya kuona kama utakuwa na tija ya kumfanya aendelee kubaki na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Rwanda, Niyonzima, aliiambia Dimba kwamba kwa sasa yupo tayari kuketi mezani na viongozi wa Yanga kuzungumzia mkataba mpya baada ya huu wa sasa kufika ukingoni mwishoni mwa msimu.

Alisema kama dili hilo mpya litakuwa na maslahi basi hataona sababu ya kuihama timu hiyo na kwamba ataendelea kukipiga katika timu hiyo iliyonyakua taji lake la 24 la ligi msimu huu.
Kumekuwa na taarifa kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo ya Yanga kwamba tayari wameshamsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka miwili, lakini kwa kauli ya mwenyewe ni kwamba yupo tayari kuendelea kubaki mahali kama tu wataweza kufikia makubaliano.

Alisema: "Kwanza nimefurahi sana kwa timu yangu kufanya vizuri. Sasa nafikiria kuketi kitako na uongozi kuzungumzia hatima yangu kuhusu suala la mkataba mpya."
Kiungo huyo amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu kabisa katika kikosi hicho cha Yanga msimu huu, ambapo kimeweza kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi uliokuwa ukishikiliwa na mahasimu wao, Simba.

Yanga, wanaonolewa na Mholanzi, Ernie Brandts, sasa wamebakiza mechi mbili kumaliza msimu, ambapo Jumamosi ijayo watakipiga na Coastal Union katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kumaliza na Simba kwenye uwanja huo, siku 18 baadaye.

No comments:

Post a Comment