Pages

Friday, April 5, 2013

FERGIE: RVP KUPUMZIKA MWIKO ATAENDELEA KURUDISHA HESHIMA YAKE YA MABAO HADI MWISHO WA MSIMU

Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza Robin van Persie atarudia hali yake ya kawaida ya kufunga Magoli na hahitaji mapumziko yeyote. 

Van Persie, mwenye Miaka 29, ameshacheza Mechi 9 sasa bila kuifungia Bao Man United.
Lakini Ferguson ana imani kubwa Straika huyo, ambae ameshafunga Bao 23 Msimu huu kwa Klabu yake, atarudia tena ufungaji.
Ferguson ametamka: "Magoli yatakuja, kila Straika hupitia Kipindi cha ukame na unategemea hilo litakwisha!"
Van Persie, ambae alijiunga Man United kutoka Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 24 mwanzoni mwa Msimu huu, amefunga Bao 19 za Ligi akikamata nafasi ya pili katika Ufungaji Bora akiwa nyuma ya Luis Suarez wa Liverpool mwenye Bao 22.
Bao la mwisho kwa Van Persie kuifungia Man United ni hapo Februari 10 walipoifunga Everton Bao 2-0.

Hata hivyo, kwenye Mechi ya Ligi Jumamosi iliyopita shuti la Van Persie ndio lililozaa Bao la ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland baada mkwaju huo kumbabatiza Beki wa Sunderland Titus Bramble na kutinga na hilo kuandikwa Bao la kujifunga mwenyewe.
Wakati huo huo, Ferguson amethibitisha kuwa Wayne Rooney, ambae hajacheza Mechi mbili sasa akijiuguza nyonga, amerudi mazoezini sasa na upo uwezekano kucheza Dabi ya Jumatatu Usiku dhidi ya Man City.
Pia, Fulbeki kutoka Brazil, Rafael da Silva, ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na nyonga, yupo mazoezini.

No comments:

Post a Comment