Pages

Wednesday, April 17, 2013

FAR RABAT WAWASILI NA MATUMAINI KIBAO






NAHODHA wa timu ya Far Rabat Bellakhdar Younes amejigamba timu yake kuifunga Azam FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika utakaochezwa uwanja wa Taifa jumamosi hii.

Younes aliyasema hayo wakati walipowasili uwanja waNdege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo huo wa raundi ya pili.

“Timu yetu ni nzuri na Azam pia ni wazuri kwani wana wachezaji waliopo kwenye timu ya taifa hivyo tutahakikisha tunafunga mabao 2-0 ili iwe rahisi wakija nyumbani”, alisema Younes.

Wachezaji wa Far Rabat ambao wapo kwenye timu ya Taifa ya Morocco ni Hammal Younes, Achchakir Abderrahim, Bellakhdar Younes, Saidi Salaheddine, Aqqal Salaheddine na Youssef Kaddior.

Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara  wa watu 31 na umefikia kwenye hoteli ya Saphire iliyoko Kariakoo.

No comments:

Post a Comment