Pages

Sunday, April 7, 2013

ERIC ABIDAL AREJEA UWANJA BARCELONA IKIUA 5-0 HUKU CESC FABREGAS AKIPIGA HAT TRICK YA KWANZA MAISHANI MWAKE

KIUNGO Cesc Fabregas jana alifunga Hat-trick yake ya kwanza maishani mwake akiiwezesha Barcelona kushinda 5-0 dhidi ya Real Mallorca na kuusogelea ubingwa wa La Liga, lakini habari kubwa ilikuwa ni kurejea uwanjani kwa Eric Abidal baada ya mwaka mmoja wa kuwa nje kufuatia kufanyiwa upasuaji wa ini.

Wenyeji jana pia walifarijika kumuona Kocha Mkuu Tito Vilanova akikanyaga Uwanja wa Nou Camp kwa mara ya kwanza tangu Januari alipokwenda kupata tiba ya saratani.
Kurejea kwa Abidal kumepokewa kwa furaha kubwa, na ilikuwa faraja wakati Mfaransa huyo anaingia kuchukua nafasi ya Gerard Pique dakika ya 70.
Happy return: Barcelona's Eric Abidal received a rousing reception
Furaha ya kurejea: Eric Abidal amepata mapokezi mazuri

Beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 33, ambaye alifaulu vipimo vya kurejea kuungana na wenzake mazoezini mwezi uliopita, ni kipenzi cha mashabiki wa Barca.
Merci: Eric Abidal akiwa amevaa fulana ya kumuenzi mpwa wake

"Namshukuru mpwa wangu, kwani bila yeye nisingekuwa hapa leo. ni wakati wa kipekee,"alisema.
Abidal anarejea katika wakati mwafaka, ambao mabeki wengine wa kati wa Barca, Carles Puyol na Javier Mascherano na beki wa pembeni, Adriano wote ni majeruhi. 
Katika mchezo huo, Fabregas ndiye alikuwa mambo yote akifunga mabao matatu peke yake, akicheza badala ya majeruhi Lionel Messi na pia akamsetia Alexis Sanchez kufunga mengine mawili.
Man of the moment: Cesc Fabregas scored his first competitive hattrick
Mkali wa sasa: Cesc Fabregas amefunga hattrick yake ya kwanza jana

No comments:

Post a Comment