Pages

Thursday, April 4, 2013

AZAM NI SAWA NA WAMESHAIFUNGA BYC NYUMBANI LAKINI WAKUMBUKE SOKA NI MCHEZO WA MAKOSA

 JANA jioni Lenzi ya Michezo ilitembelea uwanja wa Azam uliopo Chamazi kujionea maandalizi yalivyo kuelekea mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika utakaochezwa jumamosi hii uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo dhidi ya Barrack Young Controllers ya Liberia kwa Azam unaonekana kuwa mwepesi kutokana na ushindi waliupata ugenini wa mabao 2-1 wiki mbili zilizopita pia na jinsi kikosi cha BYC kinavyoonekana kwani hata walipotua uwanja wa ndege binafsi niliona kama vile wameshafungwa tena kwa idadi nyingi ya mabao.

Baada ya kufika hapo ilijionea wachezaji kila mmoja akifanya mazoezi yake kulingana na jinsi alivyojiwekea program yake.

Wapo waliokuwepo kwenye gym, wengine wakitafuta pumzi kwenye maji na wengine wakitafuta stamina uwanjani kwani program ya kocha hufanyika kila asubuhi tu.

Pamoja na wachezaji wa Azam kufanya kila mmoja mazoezi yake wapinzani wao BYC ndio walikuwa wanatumia uwanja huo kufanya mazoezi huku viongozi wao wakionekana kushangaa maendeleo ya klabu ya Azam kwani walitembezwa kila mahali.

Pia nasema Azam ni sawa na kuwa wameshafuzu japo mpira wa miguu ni mchezo wa makosa ukiteleza kidogo mwenzako anachukua nafasi kwani wanatumia kila kitu cha AZAM kuanzia maji, soda, juisi na maji ndio usiseme.

BYC ni timu ya vijana ambayo iliweza kuleta upinzani ikachukuwa nafasi kwenye ligi ya nchi yao




No comments:

Post a Comment