Pages

Sunday, April 21, 2013

ARSENAL YAIFUNGA FULHAM BAO 1-0 KWENYE EPL

JANA Arsenal wakicheza mechi yao ya 34 mchezaji wao Per Mertesacker amewapatia bao la ushindi Gunners kwa bao safi la kichwa dakika ya 43 dakika 2 kabla ya mapumziko kipindi cha kwanza, Huku Fulham wakicheza pungufu baada ya mchezaji wake Steve Sidwell  kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumkanyaga mchezaji wa Arsenal Mikel Arteta katika dakika ya 12. Arsenal nao walicheza kwa makini sana kipindi cha pili kwa kulinda bao ambalo walikuwa wameisha jipatia na kujihakikishia kutulia kwenye nafasi ya tatu, huku mchezaji wao Olivier Giroud naye akipata kadi nyekundu dakika za majeruhi 90 baada ya kufanya ndivyo sivyo. Ushindi huu unawaweka Arsenalnafasi ya tatu wakiwa na alama 63 chini ya Manchester City wenye alama 68. Fulham wao leo baada ya kufungwa wamekaa nafasi ya 11 wakiwa na pointi 40.

Per Mertesacker akishangilia baada ya kuipatia Arsenal bao dakika ya 43 dakika mbili kabla ya mtanange kwenda mapumziko.
Per Mertesacker kushoto akishangilia na huku akipongezana na Nacho Monreal
Per Mertesacker akiteleza kuingia golini baada ya kufunga bao

Mchezaji wa Fulham Steve Sidwell akimkanyaga Mikel Arteta wa Arsanal na kutupwa nje kwa kadi nyekundu
Dimitar Berbatov akichuana na Aaron Ramsey
Steve Sidwell akimkwatua Mikel Arteta

Refa Andre Marriner akimnyooshea mkono kumpa kadi nyekundu Steve Sidwell

Wasalimie...huko nje..
Berbatov akikabwa vikali na Arteta (kushoto) na Ramsey
Bacary Sagna akimtupia Kieran Richardson

Tomas Rosicky (kushoto) akiminywa na Eyong Enoh 
Olivier Giroud akimfanyia ndivyo sivyo Brede Hangeland dakika za lala salama
Bora kushinda kocha Arsene Wenger akiingia uwanjani baada ya mapumziko.

Giorud akitolewa nje dakika za lala salama
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Manolev, Senderos, Hangeland, Richardson, Emanuelson (Frei 87), Sidwell, Enoh, Kacaniklic (Petric 85), Ruiz, Berbatov.
Subs Not Used: Etheridge, Riise, Karagounis, Hughes, Rodallega.
Sent Off: Sidwell (12).
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Rosicky (Podolski 71), Arteta, Ramsey, Walcott (Wilshere 71), Giroud, Cazorla (Vermaelen 90).
Subs Not Used: Mannone, Oxlade-Chamberlain, Gervinho, Gibbs.
Sent Off: Giroud (90).
Booked: Arteta, Ramsey.
Goals: Mertesacker 43.
Att: 25,700
Ref: Andre Marriner

No comments:

Post a Comment