Pages

Friday, March 29, 2013

SIMBA KUJIULIZA KWA TOTO AFRICAN KESHO BAADA YA KIPIGO CHA KAGERA SUGAR



Kikosi cha Simba leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya mechi ya kesho dhidi ya TOTO African ya Mwanza.

Hali ya wachezaji kwa ujumla ni nzuri na mchezaji pekee aliye kambini ambaye ana hatihati ya kucheza kesho ni Haruni Chanongo, aliyeumia katika mechi iliyopita dhidi ya KAGERA SUGAR.

Amri Kiemba ambaye hakucheza mechi ya Kagera anarejea uwanjani baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake kadi tatu za njano.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig, amesema pamoja na kupoteza mechi ya Kagera, bado ana imani na vijana wake.

No comments:

Post a Comment