Pages

Friday, March 29, 2013

MASHABIKI ENGLAND WAISHTAKIWA FIFA KWA UBAGUZI WA RANGI DHIDI YA RIO FERNAND


Accused: England supporters have been reported for chants about the Ferdinand brothers - THERE IS NO SUGGESTION THAT THOSE PICTURED WERE INVOLVED
Sehemu ya mashabiki wa England katika mchezo dhidi ya San Marino.
Accused: England supporters have been reported for chants about the Ferdinand brothers - there is no suggestion that those pictured here were singing
Mtandao wa kupambana na vitendo vya kibaguzi wa rangi katika soka barani Ulaya (FARE), umeishitaki England kwa shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia mashabiki wa nchi hiyo kumshambulia kwa maneno ya kibaguzi wa rangi Rio Ferdinand na ndugu yake Anton siku ya Ijumaa, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya San Marino.

FARE wameandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa wametuma taarifa hiyo FIFA kuliarifu shirikisho hilo kuhusu kujitokeza kwa mambo ya kibaguzi katika mchezo huo, ambao England ilichomoza na ushindi mnene wa mabao 8-0 dhidi ya San Marino.

Mlinzi wa kati wa Manchester United Rio Ferdinand mwenye umri wa miaka 34, aliitwa na meneja wa England Roy Hodgson kwa ajii ya michezo miwili ya kufuzu dhidi ya San Marino na Montenegro lakini mlinzi huyo aliondolewa kikosini.

Mlinzi huyo ambaye haja itumikia timu aya taifa tangu mwaka 2011, aliondolewa kikosini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa fiti lakini badala yake akaelekea Qatar kufanya kazi uchambuzi katika televisheni ya Aljazeera.

Hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyopelekea Rio na Anton Ferdinand kukumbwa na kadhia hiyo ya kibaguzi kutoka kwa mashabiki wa England.

Mkurugenzi mtendaji wa FARE Piara Powar amesema kuwa licha ya kwamba hawakuwa na waangalizi katika mchezo huo lakini wamekusanya ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na maoni ya vyombo vya habari na kuwasilisha FIFA.

Bado chama cha soka nchini England hakijatoa maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo.

Abuse: England supporters chanted that Rio (above) and Anton Ferdinand (below left) should be 'burned'
Rio Ferdinand picha ya juu na Anton Ferdinand picha ya chini kushoto.

Anton Ferdinand (left) 

No comments:

Post a Comment