Pages

Thursday, March 28, 2013

MICHEZO YA UMISSETA WILAYA YA ILALA YAANZA KUTIMUA VUMBI LE

Shani Ally wa Benjamin akiwa na mpira

Mchezaji Marysiana Edga akijaribu kumtoka Shani Ally wa Benjamini

Wachezaji waliovaa nyekundu ni timu ya  cluster ya Benjamini na njano ni cluster ya Kinyerezi kabla ya mchezo ambao Benjamini walishind

Mchezaji Nusrat Msuya wa Kinyerezi akiwa na mpira wakati wa mchezo wao dhidi ya Benjamini kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Jangwani Wasichana
Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji kabla ya mchezo kuanza 
Mchezaji wa Benjamin akijaribu kutuliza mpira wakati wa mchezo dhidi ya Kinyerezi uwanja wa Azania
MASHINDANO ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) wilaya ya Ilala yameanza leo kwa michezo ya soka, netbali, kikapu, wavu na riadha kufanyika kwenye viwanja vya sekondari za Azania, Jangwani na Zanaki.

Kwenye viwanja vya Azania walianza kwa kufukuza upepo ambapo wasichana na wanavulana walikimbia  kwenye mbio za mita 100, 200 na 800 na washindi kupatikana.

Baadae ulifika wasaa wa soka ambapo timu za Beenjamin walicheza na Kinyerezi na mpaka Lenzi ya Michezo inatoka uwanjani hapo Kinyerezi ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 huku Cluster ya Upanga na Ilala wao wakiwa bado hawajafungana.

Kwa upande wa netbal Benjamini iliifunga Kinyerezi.

Awali akifungua mashindano hayo Mwenyekiti wa Umuja wa Wakuu wa shule za Sekondari za Ilala aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu kwenye michezo kwani kama utashindwa darasani michezo inaweza kukuajiri.

No comments:

Post a Comment