Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo kwa vyombo vya habari imesema meendeleo ya kambi na mazoezi yao mjini Arusha yanakwenda vizuri.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na afisa habari wa Simba
Ezekiel Kamwaga imesema hali ya kikosi ni nzuri morali ya wachezaji iko
juu na hakuna mgogoro au matatizo yoyote.
Paulo Ngalema. |
Kutokana na tatizo hilo, Ngalema hataweza kucheza katika ijayo dhidi ya Libolo ya Angola katika Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi ijayo.
Kupitia taarifa hiyo uongozi wa Simba umewataarifu wapenzi na washabiki wake kwamba hali ya timu ni shwari kabisa. Hakuna mchezaji yeyote aliyefungiwa wala kusimamishwa na hakuna mitafuruku baina ya wachezaji na makocha au wachezaji na viongozi wa klabu.
Simba SC pia inakanusha taarifa zozote za wachezaji wake au makocha wake kupigwa (au kutaka kupigwa) mara baada ya mechi ya Arusha.
Kwa waliokuwapo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta siku ya Jumamosi mara baada ya mechi dhidi ya Oljoro, watakuwa mashahidi kwamba baadhi ya wachezaji wa Simba walibebwa na washabiki na Mrisho Ngassa alipewa zawadi ya Sh 10,000 na shabiki mmoja kutokana na mchezo wake.
Washabiki walifahamu kuwa matokeo yale ya 1-1 yalikuwa ni sehemu ya mchezo.
Taarifa za kuwapo kwa vurugu zimetiwa chumvi kwa sababu ambazo klabu yetu haizifahamu.
Simba SC inaomba washabiki wake wawe watulivu na werevu katika wakati huu ambapo tunajiandaa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Umoja wa washabiki ndiyo utakaosaidia na si mtengamano.
No comments:
Post a Comment