Pages

Wednesday, February 6, 2013

NIGERIA NA MALI ZATINGA FAINALI AFCON KWA KISHINDO

Nigeria imeifunga mali magoli 4-1, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Afrika kwa mabao ya Elderson Echiejile alefunga magoli mawili katika dakika ya 25 na 30.

Goli la tatu limefungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.

Kipindi cha kwanza kimemalizika na sasa ni mapumziko, Nigeria ikiongoza kwa magoli 3-0.

Emmanuel Emenike

Ahmed Musa alizidi kufifisha matumaini ya Mali kucheza fainali baada ya kupachika goli la nne dakika ya 60.

Mali haikuonyesha kukata tamaa japo muda ulizidi kuyoyoma, kwani katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia bao timu yake.
Seydou Keita and Sunday Mba
Nigeria kuingia nusu fainali waliwabwaga Ivory Coast, timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kucheza fainali kutokana na ubora wa wachezaji wake.
Katika mchezo na Ivory Coast, Nigeria walishinda magali 2-1.

Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.

Nigeria fans

Timu nyingine katika nusu fainali za AFCON ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.

No comments:

Post a Comment