Goli la tatu limefungwa na Emenike katika dakika ya 44 baada ya mpira aliopiga kumgonga Momo Sissoko wa Mali.
Kipindi cha
kwanza kimemalizika na sasa ni mapumziko, Nigeria ikiongoza kwa magoli
3-0.
Ahmed Musa
alizidi kufifisha matumaini ya Mali kucheza fainali baada ya kupachika goli la
nne dakika ya 60.
Mali haikuonyesha kukata tamaa japo muda ulizidi kuyoyoma, kwani katika dakika ya 70 Cheikh Diarra aliifungia bao timu yake.
Katika mchezo na Ivory Coast, Nigeria walishinda magali 2-1.
Nayo Mali iliwatoa wenyeji wa mashindano Afrika Kusini kwa njia ya mikwaju ya penalti 3-1 baada ya timu hizo kucheza dakika 120 zikiwa zimefungana goli 1-1.
Timu nyingine katika nusu fainali za AFCON ni Ghana itakayokwaruzana na Burkina Faso. Ghana waliitoa Cape Verde katika hatua ya robo fainali kwa magoli 2-0, huku Burkina Faso wakiifunga Togo kwa goli 1-0.
No comments:
Post a Comment