Haruna Niyonzima akikabiliana na Jamali Mnyate wa Mtibwa sugar. |
Sehemu ya mashabiki wa Yanga waliohudhuria mchezo huo wakiwa wamekata tamaa baada ya kuwa nyuma kimatokeo mpaka dakika ya 86 ya mchezo huo. |
Mabingwa
wa soka Afrika Mashariki na kati Yanga ambao pia ndio vinara wa ligi
hiyo hii wameponea chupuchupu kupote mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar ya
Morogoro ukiwa ni mchezo wa mfululizo wa michezo ya ligi kuu ya soka
Tanzania bara pale walipolazimika kusubiri mpaka zikiwa zimebakia dakika
4 za muda wa kawaida kupata bao la kusawazisha.
Bao
lililo iokoa Yanga limefungwa na Hamisi Kiiza kunako dakika ya 84 ya
mchezo baada ya kupokea pasi ya Saidi Bahanuzi kutoka wingi ya kulia.
Licha
ya kutawala mchezo huo kwa sehemu kubwa, bado umakini mdogo na utulivu
wa washambuliaji wa Yanga waliokuwa wakiongozwa na Jerson Tegete ,
Kiungo Haruna Niyonzima, Simon Msuva na Didier Kavumbagu na baadaye
kuingia Hamisi Kiiza na Saidi Bhanuzi iliichelewesha Yanga kupata bao la
mapema la kusawazisha.
Mtibwa
waliaandika bao la uongozi kupitia kwa Shabani kwa kichwa baada ya
kupokea mpira wa kona kutoka kwa Issa Rashidi dakika moja kabla ya
mapumziko.
Mtibwa
iliyokuwa ikiunganishwa na Shabani Nditi, Shabani Kisiga na Rashidi
Gumbo kabla ya kutolewa ilikuwa ni kama imeridhika na bao la Kisiga na
hivyo kutumia sehemu kubwa ya kipindi cha pili kujihami hali
iliyopelekea Yanga kupanga mashambulizi kupitia pembeni kwa Msuva na
Haruna Niyonzima huku Jerson Tegete na Hamisi Kiiza wakipokea mipira
mingi sehemu ya kati ya ushambuliaji na kuwapa kazi ya ziada walinzi
Salum Swedi, Saidi Mkopi Rajabu Mohamed na Issa Rashidi kuokoa mipira
mingi katika dakiki 20 za mwisho wa mchezo.
Matokeo
hayo yanaifanya Yanga kupungunzwa kasi yake katika msimamo wa ligi
ambapo sasa ina ongoza kwa tofauti ya alama 3 mbele ya Azam fc yenye
alama 30 na Yanga ikiwa na alama 33.
No comments:
Post a Comment