Pages

Monday, February 11, 2013

CHANETA KUFANYA UCHAGUZI MACHI


Na.Mo Blog
 
Kwa mujibu wa Katiba ya CHANETA ya Mwaka 2011 ibara ya 8 kifungu namba 8.4, chama kinatangaza kuwa uchaguzi wa viongozi wa chama utafanyika Machi 23, mwaka mwaka huu  mjini Dodoma.
 
Uchaguzi huo utasimamiwa na kamati maalum itakayo teuliwa na walezi wa chama kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa.
 
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Kaimu Katibu Mkuu CHANETA Rose Mkisi (pichani), fomu zitaanza kutolewa Februari 23, mwaka huu  jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa.
 
Fumu hizo zitapaswa kurudishwa katika ofisi za BMT jijini Dar es Salaam kabla ya  machi 15, mwaka huu  saa 9 mchana.

No comments:

Post a Comment