Na.Mo Blog
Kwa mujibu wa Katiba ya CHANETA ya Mwaka 2011 ibara ya 8 kifungu namba 8.4, chama kinatangaza kuwa uchaguzi wa viongozi wa chama utafanyika Machi 23, mwaka mwaka huu mjini Dodoma.
Uchaguzi huo utasimamiwa na kamati maalum itakayo teuliwa na walezi wa chama kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na Kaimu Katibu Mkuu CHANETA Rose Mkisi (pichani), fomu zitaanza kutolewa Februari 23, mwaka huu jijini Dar es Salaam katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa.
Fumu hizo zitapaswa kurudishwa katika ofisi za BMT jijini Dar es Salaam kabla ya machi 15, mwaka huu saa 9 mchana.
No comments:
Post a Comment