Mabondia Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba
BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake
Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi
maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili
hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha
adabu
Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha
katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo
nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa
Gongo
Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa
juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu
na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini |
No comments:
Post a Comment