Pages

Friday, January 4, 2013

YANGA KIBARUANI UTURUKI LEO


Timu ya Yanga leo itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.  
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya imekuwa ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla. Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5) mfululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki.  
 Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anashukuru wachezaji wake wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo, na kwa kuwa hakuna mchezaji majeruhi atakuwa na fursa ya kumtumia mchezaji yoyote katika mechi hiyo.
 Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo utakua mgumu kwani timu ya Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Ujerumani mara kadhaa, hivyo ni timu ambayo itatoa ushindani mkubwa sana

No comments:

Post a Comment