SEMINA na kikao
cha wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa michezo na burudani
nchini, vinatarajiwa kufanyika April 12 na 13 mwaka huu, katika
jiji la Arusha.
Akizungumza katika kikao hicho, Pinto alisema TASWA inatarajia kuitisha kikao hicho, Arusha ikiwa ni sehemu ya mipango yake,kukifanya chama hicho kuwa cha kitaifa zaidi na pia kuongeza uelewa wa masuala ya michezo kwa wanahabari.
“kamati ya utendaji ya TASWA taifa hivi karibuni ilikutana ambapo pamoja na mambo mengine iliamua kuifanya kikao na semina ya wahariri mkoani Arusha hivyo nimekuja hapa ili tushauriane kuwezesha semina na kikao hiki”alisema Pinto.
Pinto alisema ili kufanikisha semina hiyo, TASWA taifa na Taswa Arusha, wanapaswa kushirikiana katika maandalizi ya kutafuta wadhamini, ambapo pia watashirikishwa wanahabari toka mikoa ya Kilimanjaro, Tanga na Manyara.
Wakizungumza katika kikao hicho, Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma na Katibu msaidizi Hamza Kalmera walieleza TASWA Arusha kuwa tayari kuandaa semina hiyo, ambayo itafanyika siku ya kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri mkuu, Edward Moringe Sokoine pia kutafanyika tamasha maalum la michezo mbali mbali.
Juma alisema TASWA Arusha itajipanga kuhakikisha wakati wa semina hiyo, wahariri na waandishi wa habari waandamizi watapata fursa ya kutembelea kaburi la Sokoine wilayani Monduli kama ishara ya kumuenzi.
No comments:
Post a Comment