|
Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo akizungumza na wanafunzi wa darasa la waamuzi | | |
|
Wanafunzi wa darasa la waamuzi wakimsikiliza mgeni rasmi Mwenyekiti wa DRFA Almas Kassongo |
|
Almas Kassongo Mwenyekiti wa DRFA akisaini kitabu cha wageni |
|
Joseph Msami, mmoja wa wanafunzi wa darasa la waamuzi akimkabidhi mgeni rasmi risala |
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Almas Kassongo leo amewaasa waamuzi kujikubali kwanza wao ndipo thamani yao inaweza kuonekana pia kwa watu wengine.
Kassongo aliyasema hayo wakati akifungua darasa la waamuzi linaloendeshwa kwenye shule ya msingi Mwananyamala B chini ya chama cha soka cha Kinondoni.
Darasa hilo lina wanafunzi 30 na linafundishwa na Mkufunzi Hemed Nteza ambaye pia alishawahi kuwa mwamuzi wa Kimataifa.
Awali wakisoma risala yao ambayo ilisoma na Jopseph Msami kwa mgeni rasmi wanafunzi hao waliomba vyama vya soka kuwaandalia semina za mara kwa mara ili waweze kuzitafsiri vema sheria pindi wanapokuwa uwanja na kupatiwa vifaa vya kuchezea.
No comments:
Post a Comment