Pages

Friday, January 25, 2013

VILABU VYAIZIDI SERIKALI, SASA KUKATA ASILIMIA 15 TU YA MAKATO YA VIWANJANI


 

Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mgawanyo wa mapato ya Uwanja wa taifa pamoja na malimbikizo ya kodi za makocha wa timu za taifa. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Juliana Yassoda, Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Silas Mwakibinga na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah. (Picha na Habari Mseto Blog)



Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Juliana Yassoda, akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari. 
Hatimaye Serikali imekubali kupunguza kiasi cha makato ya mapato ya michezo inayochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam na sasa itakuwa ikichukua asimilia 15 tu ya mapato ya michezo yote itakayokuwa ikichezwa katika uwanja huo na kwamba hakutakuwa na makato mengine yoyote zaidi ya hayo.

Hayo yamo ndani ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande tatu yaani serikali, shirikisho la soka nchini TFF na bodi ya ligi makubaliano ambayo yamesainiwa baada ya kikao cha wiki iliyopita.

Hii leo katika ofisi za wizara ya habari, utamaduni na michezo huku serikali ikiwakilishwa na naibu waziri Amos Makala na mkurugenzi wa michezo Juliana Yasoda nayo TFF ikiwakilishwa na katibu mkiuu wake Angetile Oseah na bodi ya ligi ambayo bado haijaundwa ikiwakilishwa na afisa mtendaji mkuu wake Silas Mwakibinga yamesainiwa makubaloiano hayo.

Makubaliano hayo sasa yatakuwa yanaleta unafuu kwa vilabu na timu za taifa ambazo mara kwa mara zimekuwa zikiuutumia uwanja huo katika michezo ya ligi na michuano ya kimataifa kwa ngazi mbalimbali.

Akiongea mbele ya waandishi wa habari naibu waziri wa habari Amos Makalla amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kilio cha muda mrefu na kwa kuwa serikali ni sikivu imeamua kuchukua hatua hiyo muhimu kwa kushirikiana na TFF na bodi ya ligi.

Kuhusu suala la malipo ya fedha za makocha ambazo zimepelekea akaunti ya TFF kuzuiliwa na mamlaka ya mapato nchiniTRA, Makalaa amesema suala hilo linashughulikiwa na kwamba linakwenda vizuri likiwa katika hatua za mwisho mwisho na kwamba kinacho subiriwa ni malipo ya kurudisha fedha hizo kwenye akaunti iliyofilisiwa.
Pia amesema kwamba serikali itajitahidi jambo hilo lisijirudie tena.

Pia Makalla amevipongeza vilabu vinavyoshiriki ligi kuu kwa kukubali kuingia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu unaoanza hapo kesho licha ya kwamba vinakabiliwa na mazingira magumu ya kutokuwa na fedha ambazo zimefungiwa katika akaunti hiyo ambayo ni maalumu kutunza fedha za vilabu zinazotoka kwa mdhamini wa ligi kampuni ya Vodacom.

No comments:

Post a Comment