Pages

Sunday, January 6, 2013

TWANGA PEPETA YAOGOPA MUZIKI WA KIJITONYAMA, YAKIMBIA LEADERS NA KUWAACHA MASHABIKI KIBAO

 Kipa wa timu ya Kijitonyama Veterans, Abdallah Omary (kulia) akiokoa moja ya hatari iliyoelekezwa langoni kwake, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye uwanja wa Leaders Club Kinondoni, ikiwa ni badala ya mchezo kati ya Twanga Pepeta Fc na Kijitonyama, baada ya Twanga Pepeta kuingia mitini bila kutokea uwanjani hapo, leo.
 Kipute hicho kikiendelea...
 Mapacha Hamza na Kondo wakipozi kwa picha.
Kiungo mchezeshaji wa Kijitonyama Veterans, Isihaka Mussa, akiambaa na mpira wakati mchezo huo.


TIMU inayoundwa na wanamuziki wa bendi ya African Stars' Wana Twanga Pepeta' imeingia mitini kucheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya Kijitonyama Veterans uliopangwa kufanyika Jumapili asubuhi kwenye uwanja wa Leaders Club.


Timu ya Kijitonyama Veterans ilifika uwanjani tayari kwa mchezo huo, hata hivyo wanamuziki wa Twanga Pepeta Mheshimiwa, Idd Azzan wakikosa burudani ambayo iliwatoa majumbani mwao ikikosekana.

Nahodha wa timu ya Twanga FC, Kalala Junior hakupokea simu yake pamoja na juhudi za kumtafuta  huku meneja wa  timu hiyo, Hassan 'Njoo Kesho' akisema kuwa hata yeye ameshindwa kumpata Kalala ili kujua hatma ya mchezo huo.

"Mimi nimefika hapa kwa ajili ya kuona mechi hiyo, jana (Jumamosi) wanamuziki walitangaziana, hata hivyo sijui kwa  nini, labda baada ya shoo ya jana (Jumamosi) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden na kuwafanya wachoke 
zaidi," alisema Hassan.

Kutokana na hamu mashabiki kupata burudani ya mechi hiyo, mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto  Omary aliwaomba wachezaji wanaocheza mechi za bonanza la kila siku ya Jumapili kuunda kombaini ili kucheza na Kijitonyama Veterans.

Ombi hilo lilikubaliwa na wachezaji hao ili kufanikisha kiu ya wachezaji Kijitonyama Veterans na mashabiki wa soka.

Veterans yalifungwa na Salim Sariko baada ya pasi safi ya Kiki De Kiki huku la pili likifungwa na Dastan Lwoga 

Katika mchezo huo, Kijitonyama Veterans iliifunga Kombaini ya Leaders kwa mabao 2-0. Mabao ya Kijitonyama kufuatia pasi safi ya Brian Makundi.

Wakati huo huo; katika mechi za bonanza za Leaders Club, timu ya Mango Garden iliiichapa timu ya Namaga kwa Mabao 3-1 huku Leaders ikiichapa Brake Point kwa mabao 3-1. michezo hiyo ilianza saa 4.00 asubuhi na mwingine ukianza saa 5.00 asubuhi.

No comments:

Post a Comment