Pages

Sunday, January 6, 2013

AZAM YAZINDUKA MAPINDUZI CUP, MTIBWA YANG'ANG'AMIWA NA COASTAL UNION




Ally Mohamed‘Gaucho’ akipambana na wachezaji wa Coastal Union, Othman Tamim na Suleiman Kassim ‘Selembe’ katika mchezo wa leo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. (Picha kutoka Zanzinews blog)

Michezo miwili ya michuano ya kombe la Mapindizi visiwani Zanzibar imeendelea tena, ambapo katika mchezo baina ya Mtibwa sugar na Coast Union ya Tanga mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bao 1-1.

Mtibwa ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza likitiwa nyavuni na Ally Mohamed dakika ya 57 ya mchezo nao Coast wakisawzisha kupitia kwa Jerry Santo kunako dakika ya 20 ya mchezo huo.

 MCHEZO WA PILI

Katika mchezo wa pili mabingwa watetezi wa taji la mapinduzi Azam wamechomoza na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Miembeni mchezo ambao umepigwa katika dimba la Amani.

Mabao ya Azam fc yamewekwa kimiani na Joackins Atudo kabla ya Miembeni kusawazisha bao hilo kupitia kwa Adeyoum Salehe na baadaye mshambuliaji Gaudience Mwaikimba wa Azam kuandika bao la pili kwa timu yake.

Azam ilifanikiwa kuandika bao lake la tatu katika kipindi cha pili likifungwa na
Uhuru Suleiman dakika za mwisho wa mchezo. 

Azam sasa inashika usukani kwa alama 4 ikifuatiwa na Miembeni yenye alama 3, Coastal alama 2 na Mtibwa alama 1.

No comments:

Post a Comment