Pages

Saturday, January 26, 2013

MISRI WANAUME MABINGWA WA MASHINDANO YA KIKAPU KANDA YA TANO HUKU TANZANIA IKISHIKA MKIA

Wachezaji wa Misri wanawake na wanaume wakiwa na makobe yao waliyotwaa


Nahodha wa timu ya Kenya ya Kikapu Silalei Owour akipokea kombe lao la mabingwa wa kikapu toka kwa waziri wa Habari, Vijana, utamaduni na michezo Fenella Mukangara
Kombe la Fair Play kwa timu ya Tanzania wanawake



TIMU ya Kikapu ya wanaume ya Misri imetwaa kombe la mashindano ya kikapu kando ya tano yaliyokuwa yanafanyika nchini kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.

Mashindano haya yalifunguliwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mizengo Pinda na kufungwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara yalizikutanisha nchi za mataifa saba.

Timu ya Misri imefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuifunga Rwanda vikapu 84 kwa 76 mchezo ambao ulikuwa wa ushindani na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Kenya

Ubingwa kwa upande wa wanawake ulichukuliwa na Kenya na nafasi ya pili ilikwenda kwa Misri na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Uganda.

Zawadi ya timu yenye nidhamu ilikwenda kwa Burundi wanaume na kwa upande wa wanawake ilikwenda kwa Tanzania

Mfungaji bora kwa wanaume alitoka timu ya Somalia, Fiasal Jamal aliyefunga vikapu 145 na kwa upande wa wanawake ilikwenda kwa Hilda Luvandwa.

Mchezaji bora wa mashindano ilichukuliwa na Tarek Alghanam wa Misri na kwa upande wa wanawake ilikwenda kwa Hilda Luvandwa.

Akifunga mashindano, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara alizipongeza timu zote zilizofanya vizuri na kuziomba zile ambazo hazikufanya vema zijipange ili waone pale walipofanya vibaya ili wajirekebishe.

"Hongereni wale ambao mmefanikiwa kufanya vizuri pia wale ambao hamkufanya vema chukue kama changamoto ili mashindano yajayo mje kuleta ushindani", alisema Fenella.

Timu za Tanzania wanawake na wanaume zimeshika mkia kwenye mashindano haya licha ya kufanyika hapa nyumbani


No comments:

Post a Comment