KOCHA WA YANGA ASHUKURU UONGOZI NA KUSIFU KAMBI YA UTURUKI, JUMAMOSI KUCHEZA NA LEOPARD
Kocha wa Ernest Brandts amesema
licha ya kwamba timu yake ilishindwa kupata ushindi katika ziara yake ya
mafunzo ya wiki mbili nchini Uturuki lakini ameridhika na namna vijana
wake walivyoyapokea mafundisho yake na sasa vijana hao wamekwiva kwa changamoto ya ligi kuu ya soka Tanzania bara duru la lipi.
Brandts ameshukuru uongozi kwa kuweza kuwapa nafasi ya kufanya kambi ya
maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Taznania bara kwani uwepo wao Uturuki
kwa pamoja wamepata nafasi ya kuiunganisha timu kwa pamoja.Amesema
katika michezo miwili ya mwisho vijana wake walionyesha kuiva vizuri na
kwamba amepata muda mzuri wa kukaa na vijana wake na wote wameonyesha
kuiva kimazoezi.
Amesema mazingira ya kambi yalikuwa mazuri na huduma nyingine pia zilikuwa nzuri na kwamba malengo yake yametimia.
Amerejea
kauli yake aliyotoa kabla ya kuondoka Antalya juu ya michezo mitatu ya
kirafiki aliyopata dhidi ya Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen FC kwa kusema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya
kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na
kuendelea kufanya vizuri.
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka
sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri
kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya
Arminia kusawazisha bao dakika za lala salama.
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia
timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga licha ya kwamba walipoteza mchezo huo.
kuhusu mchezo wa mwisho Brandts amesifu zaidi kuwa kikosi kilionyesha kandanda la hali ya juu dhidi ya Emmen FC ulikuwa
mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza kwamba walitawala mchezo na kupata kupata
nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake pia
kulichangia kukosa ushindi.
Mara baada ya kurejea kutoka Antalya Yanga inajipanga kwa mchezo wa kirafiki utakao fanyika jumamosi katika uwanja wa taifa dhidi ya timu ya
Black
Leopard ya Afrika Kusini ambayo inashiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment