Kikosi cha Miembeni |
TIMU ya Coastal
Union ya Tanga imetolewa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kutoka sare
ya bila kufungana na Miembani FC jioni hii kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung, Zanzibar.
Matokeo hayo Miembeni isubiri hatima yake ya kuingia Nusu Fainali katika mchezo
wa usiku wa leo kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Timu tatu
sasa zina nafasi ya kuingia Nusu Fainali, Miembeni yenye pointi nne sawa na
Azam na Mtibwa Sugar ambayo ikiwa na pointi moja sasa, ikishinda usiku
itatimiza pointi nne na mustakabali wake wa kusonga mbele utatazamwa kutokana
na wastani wake wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Tayari kutoka
Kundi A, mabingwa wa Kenya, Tusker FC wamefuzu kama vinara wa kundi hilo,
wakati Simba SC, mabingwa wa Bara wamefuzu kama washindi wa pili.
No comments:
Post a Comment