Pages

Monday, January 7, 2013

AZAM YAANGUKIA KWA SIMBA MAPINDUZI CUP NA MIEMBENI KUJIULIZA KWA TUSKER


 
TIMU ya Simba itavaana na Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi utakaochezwa Januari 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
 
Hii inatokana na  Azam kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, katika mchezo wa mwisho wa Kundi B.
  
Azam imemaliza na pointi tano na kuongoza Kundi B, ikifuatiwa na Miembeni iliyomaliza na pointi nne.
 
Miembeni itacheza na kinara wa Kundi A, Tusker ya Kenya keshokutwa kwenye mchezo wa  Nusu Fainali ya kwanza.
Katika mchezo huo, Azam ikiongozwa na washambuliaji wawili, Gaudence Mwaikimba aliyekuwa katikati na Brian Umony  alishambulia kutoka pembeni ililitia mikikimikiki mitatu lango la Mtibwa, lakini kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ alisimama imara kwa dakika zote 90 kwa kuokoa hatari zote.
 
Mtibwa nayo washambuliaji wake wawili Hussein Javu na Juma Zuilio walilitia misukosuko pia lango la Azam, lakini Mwadini Ally kipa wa Azam alikuwa makini kuokoa.
 
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, Brian Umony, Salum Aboubakar, Gaudence Mwaikimba, Humphrey Mieno na  Khamis Mcha ‘Vialli’.
 
Mtibwa Sugar;Hussein Sharif, Khamis Issa, Yusuf Nguya, Rajab Mohamed, Salvatory Ntebe, Babu Ally Seif, Vincent Barnabas, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Juma Zuilio na Ally Mohamed.

No comments:

Post a Comment