Pages

Friday, January 18, 2013

45 WAJITOKEZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TFF

WANAMICHEZO 45 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika Februari 24 mwaka huu.


Nafasi zinazowaniwa ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha kanda 13 tofauti.


Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, alisema waombaji wapya 11 ambao ni Richard Rukambura anayeomba urais wakati kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kaliro Samson, Jumbe Magati, Richard Rukambura, Omari Walii, Ahmed Mgoyi, John Kiteve, Stanley Lugenge, Francis Ndulane, Riziki Majara na Hassan Othuman Hassanoo.


Alisema mwisho wa kuchukua fomu kwa waombaji wote ni leo (Januari 18 mwaka huu) saa 10 kamili alasiri.


“Orodha kamili ya waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais). Walioomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais ni Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia.


“Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza,” alisema.


Wengine ni Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).


Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majara na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment