Pages

Tuesday, December 4, 2012

ZUKU TELEVISHENI YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA SELCOM WIRELESS PAYPOINT LEO

KAMPUNI ya Wananchi Setelite Tanzania ambao ni wasambazaji wa Zuku tv imeingia mkataba na kampuni ya Selcom Wireless paypoint kwa ajili ya kuwarahishiwa wateja wa zuku kulipia ving'amuzi vyao.

Akizungumza wakati wa kuingia mkataba huo meneja mkazi wa Wananchi Satelite Tanzania  Fadhili Mwasyeba, alisema kuwa wanafuraha kuingia ubia huu wa kibiashara kwa sababu utawarahishia wateja wao kulipia vingamuzi vyao karibu na maeneo yao kwani Selcom wameenea nchi nzima.

Naye Ofisa Uhusiano na Meneja Masoko wa Selcom Wireless Ltd, Juma Tumaini Mgoyi, alisema wanafuraha kufanya kazi na Zuku na wanaamini ni mwanzo mzuri wa kufurahia ubia huu wa kibiashara kwani wateja wake watapata huduma nzuri na karibu kwenye maeneo yao kwani wamesambaa nchi nzima.

Pia alisisitiza wakati wa kulipia unatakiwa uwe umewasha kingamuzi chako ili iwe rahisi kuunganishwa.

Pia alisema Zuku wanaendesha promotion ya Zuku tunakuthamini ambapo mteja akipeleka wateja wapya kuanzia watano atajipatia zawadi ya TV inchi 24 hadi 44 kulingana na idadi ya wateja uliowaleta.

Zuku TV wanatoa vipindi vya burudani, habari, michezo, filamu, muziki na documentary  kwa kutumia satelite na unaweza kuiona ukiwa popote Tanzania.
Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Wananchi Setelite  Tanzania ambao ndio wasambazaji wa Zuku TV akielezea jambo kwa waandishi wa Habari leo kwenye ukumbi wa Diamond, Blue Pearl Ubungo jijini Dar es salaam.

Ofisa Uhusiano na Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Selcom Wireless Ltd akielzea uhusiano wa kibiashara walioufanya na Zuku TV leo kwa wandishi wa habari.

Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Wananchi Setelite  Tanzania na Ofisa Uhusiano na Meneja wa Masoko wa Kampuni ya Selcom Wireless Ltd wakibadilishana hati ya makubaliano ya kibiashara


Waandishi wa Habari waliohudhuria hafla hiyo


No comments:

Post a Comment