Pages

Monday, December 24, 2012

TUSKER YA KENYA TAYARI YAWASILI KWA MCHEZO WA KESHO KUTWA YA YANGA.


Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto akiongea na waandishi juu ya mchezo wa kesho kutwa wa Yanga na Tusker ya Kenya uwanja wa Taifa.
George wakuganda wa Smart Sports akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mchezo wa kesho kutwa wa kimataifa wa kirafiki kati ya Yanga dhidi Tusker ya Kenya.
 Akiongea na waandishi wa habari afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema Kocha wa Yanga anatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wote katika mchezo huo ambapo Yanga itatumia nafasi hiyo kuwatumia karibu wachezaji wake wote ambapo timu hiyo inajiandaa kwa maandalizi ya safari ya kuelekea nchini Uturuki kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Baraka ametangaza kiingilio cha mchezo huo kuwa ni shilingi VIP A15,000, VIP B 10,000, VIP C 7,000 na sehemu zilizo salia itakuwa ni 5,000.

kwa upande wake George Wakuganda amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya Yanga na kwamba Yanga itatoa zawadi kwa mashabiki wake.
Aidha amesema tayari wachezaji wa Tusker wameshawasili jijini Dar es Salaam, na kwamba mashabiki waYanga wajipange kupata burudani waliyo ikosa kwa kipindi kirefu kwa timu yao.

No comments:

Post a Comment