Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto akiongea na waandishi juu ya mchezo wa kesho kutwa wa Yanga na Tusker ya Kenya uwanja wa Taifa. |
George wakuganda wa Smart Sports akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya mchezo wa kesho kutwa wa kimataifa wa kirafiki kati ya Yanga dhidi Tusker ya Kenya. |
Akiongea
na waandishi wa habari afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto amesema
Kocha wa Yanga anatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wote katika mchezo
huo ambapo Yanga itatumia nafasi hiyo kuwatumia karibu wachezaji wake
wote ambapo timu hiyo inajiandaa kwa maandalizi ya safari ya kuelekea
nchini Uturuki kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka
Tanzania Bara.
Baraka
ametangaza kiingilio cha mchezo huo kuwa ni shilingi VIP A15,000, VIP B
10,000, VIP C 7,000 na sehemu zilizo salia itakuwa ni 5,000.
kwa upande wake George Wakuganda amesema mchezo huo ni sehemu ya
maandalizi ya Yanga na kwamba Yanga itatoa zawadi kwa mashabiki wake.
Aidha
amesema tayari wachezaji wa Tusker wameshawasili jijini Dar es Salaam,
na kwamba mashabiki waYanga wajipange kupata burudani waliyo ikosa kwa
kipindi kirefu kwa timu yao.
No comments:
Post a Comment